Ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu

Tumefurahishwa na maamuzi yako ya kujiunga na Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO). Tovuti hii inaeleza shughuli na matukio mbalimbali ya chama

TUICO ni Chama cha kipekee cha Wafanyakazi hapa Tanzania. Vyama vya Wafanyakazi vimekuwa vikisukumwa na matukio mbalimbali yanayotokana na mabadiliko katika mifumo ya kijamii na kiuchumi, aidha mabadiliko ya kiuchumi yaliyoikumba nchi miaka ya 90 pia yalibadili mfumo wa Vyama vya Wafanyakazi.


Mwaka 2000 Vyama huru 11vya Wafanyakazi hapa Tanzania viliundwa kupitia Sheria ya Vyama vya Wafanyakazi Na. 10 ya mwaka 1998 na vyote vilishirikishwa katika Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA). Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) ni miongoni mwa Vyama hivyo.


TUICO ni Chama cha Wafanyakazi cha kidemokrasia kinachofanya kazi katika mazingira mapya ya uchumi wa soko huria (free market economy). TUICO inahamasisha wafanyakazi kutoka Sekta za Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri kuwa wanachama.